Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki dunia magari ya mizigo yakigongana uso kwa uso

14762 AJALI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chalinze. Watu wawili wamefariki dunia  na wengine wawili kujeruhiwa sehemu mbalimbali baada ya magari mawili  mizigo  kugongana uso kwa uso  na  kisha kushika moto katika kijiji cha Mwidu kata ya Mdaula Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani leo asubuhi,

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amewataja waliofariki dunia kuwa ni Ally Kiara (40) dereva wa moja ya magari hayo na mtu mwingine ni mwanaume ambaye bado jina lake

Nyigesa ameeleza kuwa miili ya marehemu hao imepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kusubiri ndugu kwa utambuzi na hatua zingine za mazishi.

Kamanda huyo pia amewataja majeruhi wa ajali hiyo ni Ramadhani  Idd (28) na Yasini Abdalah (24) wote wafanyabiashara na wakazi wa  Dar eslaama na wamelazwa katika kituo cha afya Chalinze kwa matibabu zaidi.

"Tunaendelea kujaribu kuzima moto eneo la tukio , lakini athari za awali ni magari hayo yameharibika, vifo na majeruhi kama nilivyokueleza, tunafanya uchunguzi zaidi wa chanzo cha ajali,"amesema Kamanda Nyigesa.

Chanzo: mwananchi.co.tz