Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki dunia ajali ya lori Njombe

Njombe Ajali Lori.png Wawili wafariki dunia ajali ya lori Njombe

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili akiwemo dereva wa lori wamefariki dunia baada gari hilo kupinduka katika eneo la Lihogosa lililopo halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoid Banga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Ijumaa Aprili 19, 2024.

Kamanda Banga amesema chanzo cha ajali hiyo ni lori lilikwaruzana na lori lingine la makaa ya mawe likiwa linatokea Makambako kuelekea Songea na kisha kupinduka.

"Dereva wa lori la mbao alipoteza maisha papo hapo pamoja na mmiliki wa mzigo wa mbao, lakini utingo wa lori ni majeruhi na amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Njombe," amesema Banga.

“Mpaka sasa dereva wa lori la makaa ya mawe hajakamatwa ili ahojiwe kuhusu ya ajali hiyo,”ameongeza Kamanda Banga.

Waliofariki dunia ni dereva wa lori hilo Bryson Kihombo (30) na Juma Joseph (43) mmiliki wa mzigo wa mbao ambazo zilikuwa zikisafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live