Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki dunia ajali ya gari na baiskeli Kiteto

Akutwa Akiishi Na Maiti Ya Mumewe Ndani Wawili wafariki dunia ajali ya gari na baiskeli Kitetod

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi wilayani Kiteto, mkoani Manyara linamshikilia dereva wa gari aina ya Mistubishi, Haruna Salumu (35) mkazi wa Kibaya kwa tuhuma za kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwa kwenye baiskeli moja kwa kuwagonga kwa gari.

Taarifa hizo zinasema marehemu walikuwa wanaingia barabara kuu, waligongwa na gari hiyo iliyokuwa ikitokea makao makuu ya Wilaya ya Kiteto, Kibaya, kuelekea kata ya Sunya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Manyara, ACP George Katabazi akizungumza na Mwananchi Digital leo, Jumapili Novemba 12.2023 amewataja marehemu hao kuwa ni dereva baiskeli, Matonya Lemtya (59) na abiria wake David Mayai (15) wote wakazi wa Logoit wilayani Kiteto.

“Chanzo cha ajali ni, Matonya Lemtya (59) mwendesha baiskeli, huyu aliyekuwa amepakia abiria aliingia barabara kuu ghafla bila tahadhari wakitokea kwenye chochoro na kugongwa na gari hilo,” amesema ACP Katabazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live