Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki ajali Same

Ajali Same Ajali Wawili wafariki ajali Same

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: mwanachidigital

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni mume na mke wamefariki dunia papo hapo katika Kijiji cha Kijomu, Kata ya Hedaru Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi la Kilimanjaro Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam na kugongana na gari dogo ambalo lilikuwa na watu wawili ambao wote wamefariki dunia.

Akizungumza, Mtendaji wa Kijiji hicho ambaye alikuwa eneo la ajali, Veran Mtenga amesema ajali hiyo imetokea leo Juni 23, saa 12 asubuhi katika Kijiji hicho.

"Baada ya kupata taarifa saa 12, asubuhi nilifika eneo la tukio, nilikuta basi la Kilimanjaro na gari dogo ambalo lilikuwa limeharibika vibaya, kwenye gari dogo kulikuwa na watu miwili, mwanamke na mwanaume ambao walifia hapo hapo, "

Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilmanjaro, Simon Maigwa kujua chanzo cha ajali hiyo hazikuzaa matunda licha ya kupigiwa simu na kutaka atumiwe ujumbe wa SMS kwa kuwa yupo kwenye kikao.

Chanzo: mwanachidigital