Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafariki, 15 wanusurika kifo baada ya kula chakula cha sumu

Mwaiba Ed Wawili wafariki, 15 wanusurika kifo baada ya kula chakula cha sumu

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, wakati akizungumza na waandishi wa habari, amewataja waliofariki kuwa ni Manyirizu Joseph (6) na Bertha Mateso (5) ambao wote ni wakazi wa Ikobe wilayani Mbogwe.

Kamanda Mwaibambe amesema watoto hao na wengine waliojeruhiwa walikula mabaki ya chakula (kiporo) ambacho ni wali na nyama ya kondo na kuanza kutapika pamoja na kuharisha.

Aidha, Kamanda huyo amesema hali ya manusura wanaendelea na matibabu katika kituo cha afya Iboya wilayani Mbogwe mkoani humo na hali zao zinaendelea vizuri.

Chanzo: ippmedia.com