Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafa ajalini, mwingine ajinyonga kwa waya

267493ba39b7ae39f4efa9c6f3c00667 Wawili wafa ajalini, mwingine ajinyonga kwa waya

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Katavi, akiwamo mkazi wa Mtaa wa Kwalakwacha katika Manispaa ya Mpanda, Twaibu Omar (24), aliyejinyonga kwa waya hadi kufa akiwa bafuni.

Aidha, wafanyakazi wawili wa basi la abiria waliopoteza maisha huku abiria 10 wakinusurika kufa baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamini Kuzaga, alisema matukio hayo ni ya Septemba 30 mwaka huu katika maeneo tofauti.

Kuhusu aliyejinyonga, Kamanda Kuzaga alisema mkasa huo ulitokea saa 8:30 mchana katika Mtaa wa Kwalakwacha uliopo Kata ya Nsemulwa, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Alisema Omar aliingia bafuni na kujitundika kitanzi cha waya hadi kufa na mwili wake ulikutwa ukining’inia kwenye kenchi. Hakuacha ujumbe.

Kuhusu ajali iliyosababisha vifo vya wafanyakazi wawili wa basi la abiria, aina ya TATAMarcoporo lenye namba za usajili T827 CUG, Kamanda Kuzaga alisema ilitokea saa 8:15 mchana katika eneo la Lyamgotoka lililopo katika Kitongoji cha Majengo A katika Kijiji cha Songambele, Kata ya Kapalamsenga wilayani Tanganyika.

Aliwataja waliokufa ni kondakta wa basi hilo, Kivoga Thabiti (38) na utingo Shaban Issa (30) wote wakazi wa mjini Mpanda.

Abiria walionusurika ni Maria Silvester (60) mkazi wa Tulieni, Joseph Jacob (57) mkazi wa mjini Mpanda, Ester James (57) mkazi wa Kijiji cha Itetemya na Hadija Mkumbi (50) mkazi wa mjini Mpanda.

Wengine ni Zainabu Almasi (48) na Rashidi Jackson (32) wakazi wa Kijiji cha Ikola, John Mkungu (37), Geoffrey Malingumu (37) na Salome Paul (14) wakazi wa Kijiji cha Karema na Regnald Maiko (30) mkazi wa Kijiji cha Kapalamsenga.

Alisema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria, TATA aina Marcoporo yenye namba za usajili T 827 CUG mali ya mfanyabiashara wa mjini Mpanda, Humud Zahor.

Lilikuwa likiendeshwa na Daniel Ulaya (32) mkazi wa Mtaa wa Kawajense mjini Mpanda.

Alisema chanzo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva aliyeshindwa kulimudu katika kona. Dereva alikimbia na anasakwa na polisi sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo: habarileo.co.tz