Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafa ajalini mkoani Kilimanjaro

65585 Ajali+pic

Fri, 5 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Watu wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro  baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuligonga kwa nyuma gari jingine lililokuwa limeegeshwa barabarani.

Waliofariki katika ajali hiyo ni mtawa wa kanisa Katoliki, Octavian Richald mkazi wa Rombo na Aminiel Christopher, dereva wa gari hilo aina ya Toyota Landcruiser lililokuwa likitokea Lushoto mkoani Tanga kuelekea Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Julai 3,2019 eneo la Mgagao barabara kuu Mwanga- Same.

"Gari hiyo ilikuwa ikitokea Lushoto na iliigonga gari jingine aina ya Tata iliyokuwa imeegeshwa barabarani. Abiria katika gari hilo walifariki hapohapo,” amesema akibainisha kuwa chanzo ni mwendokasi wa Landcruiser hiyo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz