Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wafa ajalini Pwani

15512 Wawili+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Chalinze. Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso katika barabara ya Dar es Salaam- Morogoro leo Jumanne Setemba 4, 2018.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Howo mali ya kampuni ya kokoto ya Gulf Agent iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kwenda Chalinze na gari aina ya DAF mali ya Kampuni ya RAS Logistic (T) Ltd iliyokuwa inatokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam.

Akizungumza leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema ajali hiyo imetokea kijiji cha Mbala.

Amesema katika ajali hiyo waliofariki ni dereva na utingo wa gari la DAF na majina yao hayajafahamika kwa kuwa hawakuwa na kitambulisho chochote.

Amesema majeruhi ni Ramadhan Kibingo (38) ambaye ni dereva na utingo wake Ibrahimu Said (28) wote wakazi wa Dar es Salaam.

“Ni kweli imetokea hii ajali na kama nilivyokueleza madhara yake ni vifo, majeruhi pamoja magari yote kuharibika," amesema Nyigesa.

Kamanda huyo wa Polisi Pwani ameongeza kuwa miili ya marehemu imepelekwa Hospital ya Rufaa Tumbi kwa uchunguzi na majeruhi wamepelekwa kituo cha afya Chalinze kwa matibabu na hali zao zinaendelea vema.

Nyigesa amebainisha kuwa dereva wa gari la Howo anashikiliwa na polisi katika kituo cha afya Chalinze anakopatiwa matibabu.

"Chanzo cha ajali ni dereva wa Howo kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso na gari aina ya DAF kwa hiyo huyu bado tunamshikilia na afya yake ikiimarika tutamfikisha mahakamani," amesema Nyigesa.

Chanzo: mwananchi.co.tz