Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji waonyeshwa maeneo ya uwekezaji mkoani Mtwara

66661 Uwekezajipic

Sun, 14 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Baadhi ya wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania walioshiriki kongamano la kimataifa la uwekezaji katika sekta ya ubanguaji wa korosho wanatembelea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.

Kongamano hilo linalofanyika mkoani Mtwara limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Akizungumza na wawekezaji hao leo Jumamosi Julai 13, 2019 katika ziara ya kutembelea maeneo hayo, mkuu wa Mkoa wa Mtwara,  Gelaius Byakanwa amesema wapo tayari kupeleka huduma muhimu za umeme, maji na barabara katika maeneo ambayo watu watakuwa na nia ya kuwekeza.

“Akijitokeza mtu akasema anachukua eneo kwa ajili ya uwekezaji, ofisi yangu, Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania), Tarura (Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini) pamoja na mamlaka ya maji tunaanza haraka kuweka miundombinu ya msingi,” amesema.

Byakanwa amesema Mkoa huo una ardhi nzuri na inapatikana kwa gharama nafuu.

“Tumeonyesha njia watakaovutiwa mje tunawakaribisha, tuna huduma za usafiri wa anga, barabara na bandari,” amesisitiza.

Pia Soma

Maeneo waliyoonyeshwa kwa ajili ya uwekezaji ni pamoja ya yaliyo pembezoni mwa Bahari ya Hindi kwa ajili ya hoteli na maeneo ya uwekezaji wa viwanda.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz