Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavuvi waomba kupelekewa chanjo ya Uviko 19

Uviko Pc Data Chanjo

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Wavuvi wa ziwa Victoria kutoka visiwa 14 vilivyo wilayani Sengerema wameiomba Serikali kuwapelekea chanjo ya Uviko 19 visiwani humo kutokana na kituo cha kutolea chanjo hicho kuwa mbali na maeneo yao.

Mwenyekiti wa Wavuvi kisiwa cha Gembale, Hassan Mhenga amesema watu wanashindwa kuvuka ziwa kwenda zahanati ya Lushamba kupata chanjo ya Uviko 19, hivyo kuwalazimu kutumia gharama kubwa ya usafiri.

Amesema kama huduma hiyo itafikishwa kwenye Visiwa hivyo watu wengi watajitokeza kupata chanjo hiyo ya Uviko 19 na kujikinga na maradhi hayo.

“Serikali inatakiwa kupeleka chanjo huko Ili kuwasaidia wavuvi," amesema Mhenga.

Mmoja wa Wavuvi Kisiwa cha Nyamango Saimoni Kube amesema wako tayari kupata chanjo hiyo kama Serikali itaona umuhimu wa kuwafikisha huduma hiyo kwenye maeneo yao ya kufanyia kazi.

Serikali imetenga Vituo vya kutolea chanjo ya Uviko 19 sehemu mbalimba lakini imesahau kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo ya visiwani.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bulyaheke Jonathani Kuditha ambayo kata yake inamiliki Visiwa 14 amesema wao wamekwishaliona hilo atapeleka maombi hayo kwenye Mamulaka husika Ili kuona namuna ya kuwasaidia.

Chanzo: Mwananchi