Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavuvi wagoma, washinikiza Serikali kukomesha mauaji ya wenzao

38811 Wavuvi+pic Wavuvi wagoma, washinikiza Serikali kukomesha mauaji ya wenzao

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Fungamano la vyama vya sekta ya uvuvi wa ukanda wa Pwani Tanzania limetangaza mgomo wa wavuvi kuishinikiza Serikali ya Tanzania kukomesha mauaji ya wavuvi baharini.

Akisoma tamko la pamoja leo Jumatatu Januari 28, 2019 mwenyekiti wa Fungamano hilo, Mohammed Said amesema  mbali na kuuawa, wavuvi wamekuwa wakikumbana na mateso mbalimbali, vipigo na kuzuiwa kutumia nyavu zenye matundu madogo.

Said amesema wanamuomba Rais John Magufuli kwenda kuwasikiliza madai yao.

Katika kikao hicho kilichokuwa kikiendelea hadi ilipofika saa 6:20 mchana katika soko la Feri jijini Dar es Salaam, Said amesema hawatavua samaki wala kufanya shughuli yoyote hadi pale Serikali itakapotoa tamko kuhusu unyanyasaji wanaoupata.

Amesema unyanyasaji huo unafanywa na Idara ya Uvuvi, huku wavuvi kutoka ukanda wa Pwani wakitoa ushahidi jinsi wanavyotozwa faini, kupigwa na kunyanyaswa na baadhi ya watendaji wa Idara ya Uvuvi na askari.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz