Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavuvi Bukoba wapatiwa mafunzo na vifaa

Wavuviii Ww Wavuvi Bukoba wapatiwa mafunzo na vifaa

Tue, 29 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wavuvi kutoka katika wilaya za Missenyi na Bukoba wanaoshiriki mafunzo ya uokozi yaliyotolewa na serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, wameahidi kutumia mafunzo hayo kuokoa watu kitaalamu tofauti na awali ambapo waliokoa kwa kutumia uzoefu wa maji.

Wavuvi hao wapo waliohusika kwenye uokozi wa ajali ya ndege iliyotokea Novemba 6 mwaka huu, na wale ambao hawakuhusika.

Baada ya mafunzo ya nadharia kwa wavuvi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, baadaye walikwenda eneo la Gymkhana na kufanya mafunzo kwa vitendo katika Ziwa Victoria, kwa kutumia baadhi ya vifaa walivyopewa na serikali ikiwamo maboya, na baada ya mafunzo hayo wavuvi hao wakaishukuru serikali kwa kuwaongezea maarifa.

"Umakini na usalama wetu ndio ilikuwa changamoto kwetu, sasa tumepata mafunzo tumeelewa kwamba kabla ya kuokoa mtu inabidi kujua namna ya kujiokoa mwenyewe na kujihakikishia kama mazingira ya kuokoa yapo salama, tunamshukuru Mungu tumeongeza uwezo na ikitokea ajali yoyote tupo tayari kusaidia" wamesema wavuvi hao

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa kwa wavuvi, Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila, amesema kuwa vifaa walivyopewa wavuvi hao vinawaondoa katika mazingira ya kufanya kazi kwa mazoea ya kuokoa bila kuwa na vifaa vya kuwasaidia.

Kutolewa kwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alilolitoa baada ya kutokea kwa ajali ya ndege ya shirika la Precion Air, iliyotokea Novemba 06 mwaka huu, na kusababisha vifo 19 na majeruhi 26, huku wavuvi wakionekana kuwa na msaada mkubwa katika kuokoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live