Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavamizi vyanzo maji Kilimanjaro kushughulikiwa

Kilnjro.jpeg Wavamizi vyanzo maji Kilimanjaro kushughulikiwa

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti watu waliovamia eneo lenye chanzo cha maji Njoro ,kata ya Miembeni wilayani humo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu huyo wa mkoa kupata taarifa,kutoka kwa diwani wa kata hiyo,Mohamed Mushi kuwawapo baadhi ya watu wanauza viwanja Sh5 milioni eneo karibu na chanzo hicho cha maji.

Akizungumza mara baada ya kufika katika chanzo hicho cha maji,amesema hatakubali kuvumilia wala kuona vyanzo vya maji vikiharibiwa na kuhujumiwa na watu wachache ambao wana nia ovu ya kudhulumu mali za serikali ambapo ameagiza wachunguzwe na kuchukuliwa hatua.

"Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa Muwsa naagiza haya maeneo lazima tuyalinde maana hii changamoto ya maji tunayoipitia sasa hivi ni kwasababu maeneo mengi tumeyaachia tuu,haya maeneo ya vyanzo vya maji lazima tuwe nayo makini,"amesema Kagaigai

"Kwa haraka sana chochote kinachofanyika hapa naomba kusimame,ikiwezekana RPC tumieni polisi kuwaondoa wavamizi kwenye hivi vyanzo ili tuhakikishe tunalinda haya maeneo vinginevyo tutapata shida ,na mimi siwezi kukubali,"

"DC tumia hata polisi kwa mtu atakayejenga kwenye vyanzo vya maji ,vyanzo hivi vya maji vinatakiwa kulindwa ,naomba ufuatilie kuona ni kwa kiasi gani huyu mtu anamiliki hili eneo ambalo anauzia watu ,"amesema RC Kagaigai

Chanzo: www.tanzaniaweb.live