Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waumini waliofungwa kwa kukataa chanjo ya surua waachiwa huru

Kufungwa Sac Waumini waliofungwa kwa kukataa chanjo ya surua waachiwa huru

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga imewaachia huru Wachungaji na Waumini saba wa Kanisa la Watch Tower Wilayani Kalambo waliohukumiwa kifungo cha Mwaka mmoja jela kwa kosa la kuzuia Watoto walio chini ya umri wa Miaka mitano kupewa chanjo ya kuzuia Ugonjwa wa Surua na Rubella.

Imefahamika kuwa hukumu iliyotolewa kwa Waumini hao ambao walishtakiwa katika Mahakama ya Mwanzo kisha adhabu ya kwenda jela kuthibitishwa na Mahakama ya Wilaya, ilikuwa na dosari za Kisheria.

Baadhi ya dosari ni kuwa Waumini walidaiwa kugomea amri lakini haikubainishwa waligomea amri ya nani kati ya mhudumu wa Afya aliyekuwa akitoa chanjo na Mamlaka ya Serikali na pia hawakupewa nafasi ya kujitetea katika shtaka hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live