Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wauguzi wagoma kumtibu mzee sababu ya viatu

Viatu Matibabu Wauguzi wagoma kumtibu mzee sababu ya viatu

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wahudumu wa kituo cha afya kata ya Bunduki waligoma kutoa matibabu kwa bibi mmoja anaejulikana kwa jina la Laurentina France kwa sababu bibi huyo hakuvaa viatu wakati anafika kutaka kituo hicho ili kupata matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigela, alipofika katika kata hiyo bibi huyo alisema alifika katika hospitali hiyo kwaajili ya kupata matibabu ya kushusha presha lakini cha kushangaza wahudumu wa zamu aliowakuta waligoma kumpa matibabu huku wa kisisitiza bibi huyo kuvaa viatu kwanza ndipo atibiwe.

Kufuatia hali hiyo majirani wa bibi huyo walichukua jukumu la kuchukua bibi huyo kisha kumpeleka katika zahanati ya kata jirani alikofaniniwa kutibiwa.

Baada ya kueleza kadhia hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigela akatoa onyo kwa watumishi wa serikali sekta zote ambao hawana weledi katika kazi kuacha tabia hizo mara moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live