Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi wawili Tarura wafariki ajalini, RPC awataja majina

64271 Tarura+pic

Tue, 25 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Wafanyakazi wawili wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) Mkoa wa Songwe wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Hilux na Fuso.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC), Juma Bwire amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 11 alfajiri katika kata ya Izazi Tarafa ya Isimani mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dodoma.

Bwire amesema gari aina ya Toyota Hilux mali ya Tarura iliyokuwa ikiendeshwa na Lodrick Ulio (35) likitokea Iringa kwenda Dodoma liligongana uso kwa uso na gari aina ya Mistubish Fuso mali ya Wilison Msenga likitokea Dodoma kwenda Iringa.

Amewataja walifariki katika ajali hiyo ni Lodrick Richard (35) dereva wa Tarura na Joyce Mlay (45) wote wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Majeruhi katika ajali hiyo ni Ernest Mgeni (49), Gervas Myovela (44) Jamadin Mikata (32).

“Majeruhi wote wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa matibabu zaidi na miili ya marehemu imekabidhiwa kwa meneja wa Tarura manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuipelekwa Dodoma tayari kwa utaratibu wa mazishi,” amesema

Pia Soma

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa ni uzembe wa dereva wa fuso kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhama upande mmoja na kugongana uso kwa uso na gari ya Tarura.

“Dereva wa fuso ambaye amejulikana kwa jina moja la Amosi amekimbia baada ya ajali  na jeshi la polisi linamtafuta.”

“Pia, napenda kutoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia barabara waheshimu sheria na watumiaji wengine wa barabara,” amesema Bwire

Chanzo: mwananchi.co.tz