Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi watano wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Dorothy Gwajima 4 640x400 Watumishi watano wasimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Watumishi  watano kati ya sita wa Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa vyombo vya maadili ya utumishi wa umma pamoja na mabaraza na bodi za kitaaluma.

Watumishi hao tayari wamefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa dawa zenye thamani zaidi ya Milioni 200 na  mmoja wao alikiri na kuhukumiwa kulipa Milioni 100 na waliobaki walirejeshwa kazini.

Hata hivyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima hivi karibuni aliagiza watumishi hao kusimamishwa kazi kufuatia Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Cornel Magembe kudai kuwa  hakuridhishwa na watumishi hao kurejeshwa kazini kwani hawaaminiki tena kwenye utumishi wa umma na kamwe haiwezekani na haieleweki inawezekanaje mtumishi wa umma aibe halafu akishalipa anarejeshwa kazini.

MAGUFULI AMVAA KITILA MKUMBO HADHARANI “NILIKOSEA KUCHAGUA VIONGOZI, KWAKO WANAFUNZI WANAKAA CHINI”

Chanzo: millardayo.com