Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi wanne watumbuliwa kwa Uhujumu wa Pembejeo

FD5F193E CFB3 4431 B671 3EDA5242C50D 660x400.jpeg Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumishi wanne wa serikali wakiwemo maafisa kilimo wawili kutoka wilaya Tandahimba Mkoani Mtwara wamesimashiwa kazi kwa tuhuma za kujaribu kuhujumu zoezi wa ugawaji wa pembejeo ambazo zinatolewa bure na serikali kama ruzuku kwa wakulima wa korosho nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti amesema hayo wakati akishuhudia ushushwaji wa salpha ya unga tani 5632 kutoka kwenye meli bandarini Mtwara.

Gaguti amesema watuhumishi hao ni miongoni mwa watu 12 ambao wanashikiliwa na vyombo vya ulinzi kwa kosa la kujaribu kuchepushwa Lita 400 za salpha ambayo serikali ilitoa Kama ruzuku kwa wakulima wilayni humu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live