Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi wanne wakamatwa Handeni, wananchi 27 wasakwa

RC MgumbaC8AC.jpeg Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akuzungumza na Wananchi

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi limewakamata viongozi wanne wa Serikali wilayani Handeni mkoani Tanga kwa tuhuma za kuuza ardhi ekari zaidi ya 500 na mbao 1,000 kinyume na utaratibu.

Viongozi hao wamekamatwa leo Jumapili Novemba 13, 20 kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba.

Mgumba ametoa agizo hilo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kwamsisi kusikiliza kero za wananchi ambapo amesema viongozi hao wametumia vibaya madaraka yao.

Pia, mkuu huyo wa mkoa ameagiza kukamatwa wananchi 27 ambao wapo kwenye orodha ya kudai kununua mashamba lakini hawako kihalali ila wametengenezwa na viongozi.

Viongozi waliokamatwa ni Mtendaji wa Kata ya Kwamsisi, Eric Chipindula, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwedikabu, Rajabu Makamba, Mtendaji wa Kijiji hicho Zahara Sempule na Ofisa Misitu wa wilaya Elinihaki Mdee.

"Takukuru fuatilieni hili suala lakini polisi kamateni hawa viongozi wote na wapelekwe ndani kwaajili ya mahojiano zaidi kwani wameshindwa kutumia vizuri nafasi zao", amesema Mkumba.

Viongozi wa vijiji hivyo wanatuhumiwa kwa nyakati tofauti kuuza zaidi ya ekari 500 za ardhi pamoja na kutumia vibaya madaraka yao.

Awali mkazi wa Kwamsisi Bakari Ramadhani mbele ya mkuu huyo wa mkoa amesema kwenye eneo hilo la Kwamsisi, maeneo mengi ya serikali yameuzwa na viongozi, lakini hakuna hatua zimechukuliwa.

Chanzo: Mwananchi