Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi waliopandishwa madaraja Simanjiro watakiwa kuongeza juhudi

60336 Pic+madaraja

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Yefred Myenzi amewataka watumishi 384 waliopandishwa daraja kuongeza juhudi na ufanisi katika kazi.

Myenzi ametoa kauli hiyo jana Jumanne Mei 29, 2019  wakati akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Mirerani Benjamin Mkapa kuhusu watumishi hao kupandishwa daraja.

Myenzi amesema kati ya watumishi hao 384, 377 wamepandishwa madaraja na wengine saba wamebadilishwa madaraja waliyokuwa nayo awali.

Amesema watumishi hao wa idara na vitengo tofauti ikiwemo walimu, afya, kilimo na utawala ambao ni wa ngazi ya watendaji wa vijiji na kata, manunuzi, uchaguzi na mipango.

"Watumishi hao wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kuanzia Mei, 2019 wamepandishwa madaraja kwa kuingizwa kwenye mfumo kupitia maboresho waliyofanyiwa upya," amesema Myenzi.

Amewataka watumishi wengine ambao hawakupata nafasi kwa wakati huu kuongeza juhudi ya kazi na zitaonekana.

Pia Soma

Ofisa elimu Sekondari wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Augustine Bayo amempongeza hatua hiyo ya upandishaji madaraja kwa maelezo kuwa itachochea utendaji kazi hasa kwa walimu.

Mkuu wa shule hiyo, Samwel Kaitira amemshukuru mkurugenzi huyo kwa kuchukua hatua hiyo kwa maslahi ya watumishi.

Chanzo: mwananchi.co.tz