Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi, makada CCM Mbeya waandamana kumpongeza Magufuli

48189 Maandamanopic

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Watumishi wa Serikali mkoani Mbeya na wanachama wa CCM leo wamefanya maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake wa kazi.

Maandamano hayo yameongozwa na viongozi waandamizi wa chama hicho tawala na kupokewa katika ofisi za CCM wilaya na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika na mkurugenzi wa jiji la Mbeya, James Kasusura.

Pia walikuwapo wanafunzi wa shule zaj ya wazazi ya CCM, maofisa usafirishaji na wapiga debe katika vituo vya mabasi vya Uyole, Nanenane, Kabwe na stendi kuu.

Maandamano hayo yalianzia  viwanja vya Ruanda Nzovwe hadi ofisi hizo za CCM.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz