Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi Namtumbo wadai posho kwa miezi 5

Ee98561ccfbe27d3db6c3ba260863bb0.png Watumishi Namtumbo wadai posho kwa miezi 5

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WATUMISHI mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo iliyopo Mkoa wa Ruvuma walioshiriki zoezi uandikishaji vyeti vya kuzaliwa vya watoto wamelalamikia kusotea posho zao kwa zaidi ya miezi mitano sasa .

Watumishi hao wanasema wanadai posho ya zaidi ya Sh milioni 100 na juhudi zao za kuzidai zinaelekea kugonga mwamba.

Pamoja na kudai kuwa hawajalipwa fedha hizo wanasema katika zoezi zima wamelipwa posho ya wiki 2 na hawajalipwa tena.

Walieleza kuwa hata wanapofuatilia malipo hayo kwa uongozi huambiwa wasubiri mpaka watakapoitwa kwa barua na kwamba wamsubiri hadi sasa imepita miezi mitano hawajaitwa wala kuonekana dalili za kulipwa.

Aidha walieleza kuwa kwa taarifa walizonazo ni kwamba fedha hizo zimebadilishiwa matumizi.

Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Evans Titus licha ya kukiri watumishi hao kuidai halmashauri hiyo alikanusha taarifa za mabadiliko ya matumizi ya fedha hizo na kwamba

kuchelewa ni sababu za kimfumo.

Titus aliwataka kuvuta subira na kwamba suala lao linashughulikiwa ili waweze kulipwa posho hizo.

Chanzo: habarileo.co.tz