Tue, 19 Sep 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ameagiza watumishi 7 wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi kuchukuliwa hatua, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, hali ambayo imedaiwa kuzorotesha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za Halmashauri hiyo.
Mchengerwa ameyasema uamuzi huo wakati wa ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa, kuanzia sasa Maafisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhirifu wasihamishwe vituo kwenye vituo vyao vya kazi mpaka mashauri yao yanapokamilika.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live