Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi 45 wafukuzwa kazi Tanga

73636 Watumishi+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga nchini Tanzania limeridhia kufukuzwa kazi watumishi 45 ambao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kiutumishi.

Mwenyekiti wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Handeni Mustafa Beleko amesema leo Ijumaa Agosti 30, 2019 kuwa watumishi hao wamekutwa na makosa mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo kusema uongo, kughushi vyeti na utoro kazini.

Amesema watumishi 10 wamefukuzwa kazi kwa kutoa taarifa za uongo kwenye masuala ya kiutendaji, 24 wameghushi vyeti, saba wamejipatia ajira bila kufuata mfumo wa ajira na wanne wamefukuzwa kwa sababu ya utoro kazini kwa kuondoka kwenye maeneo ya kazi bila ruhusu zaidi ya mara tano.

"Pia wapo wengine wawili ambao wamepewa adhabu za kiutumishi kwa makosa mbalimbali ikiwemo upotevu wa fedha ila makosa yao hayakusababisha wao kufukuzwa kazi," alisema Beleko.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz