Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi 15 Dar kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka

MAHAKA HI 1 Law Watumishi 15 Dar kizimbani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyakazi 15 wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwemo wahasibu, ofisa afya, mweka hazina na ofisa mtendaji wa mtaa, wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 143 yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Halmasahuri ya Jiji la Dar es Salaam kiasi cha Sh8.9 bilioni.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo jioni, Juni 26, 2023 na Wakili wa Serikali, Faraji Ngukah akisaidiana na Pendo Temu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Wakili Ngukah amedai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Julai Mosi 2019 na Juni 6, 2021 Katika jiji la Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu na kujipatia Sh8.9 bilioni, mali ya Halmashauri ya Jiji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live