Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi 10 walihamisha fedha kinyemela Kigoma

Serikali Kufufua Viwanda Vya Korosho   Majaliwa.png Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amepokea taarifa ya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo imebainika watu 10 wanahusika na mtandao wa uhamishaji fedha kinyume cha taratibu.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo leo Oktoba 25, 2023, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma ni lazima atunze na kuratibu vizuri matumizi ya fedha zinazopatikana.

"Taarifa nimeipokea na mapendekezo ya kamati wote tumeyasikia, hatua za haraka zichukuliwe kwa sababu Mheshimiwa Rais anatafuta fedha za kuleta maendeleo lakini kuna watu wachache wanafanya ubadhirifu," amesema Waziri Mkuu

Amewataka Mawaziri na Makatibu Wakuu wasiridhishwe na taarifa za miradi wanazopokea pindi wakiwa ziarani kwani licha ya kuwa kuna wataalamu wanatoa taarifa nzuri mbele ya viongozi hao, bado kuna tricks wanachezacheza.

Akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Kigoma, Septemba 20-22, mwaka huu, Waziri Mkuu alipata taarifa ya uwepo wa fedha zilizoingizwa kwenye akaunti ya Amana ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kutoka TAMISEMI na kisha fedha hizo kuondolewa baada ya muda bila maelekezo maalum wala kujua zilitumikaje.

"Hapa Manispaa mnapokea fedha, zinakaa kwenye akaunti kwa muda halafu zinapotea, hazijulikani zimefanya nini, nitaleta timu, waje wafuatilie hapa Kigoma, waende hadi TAMISEMI ili tuone huo mnyororo unaenda wapi,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na viongozi wa dini, Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma na Halmashauri ya wilaya ya Kigoma kwenye ukumbi wa NSSF, Kigoma mjini Septemba 22, mwaka huu.

Mapema, akitoa taarifa kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa timu ya uchunguzi, alisema timu hiyo ilibaini kuwa uchepushaji wa fedha hizo unafanyika kwa kutumia njia kadhaa ikiwemo kuomba kibali kutoka Hazina cha kuvuka na bakaa ya fedha za miradi mwaka wa fedha unapokaribia kwisha.

"Timu ya uchunguzi imebaini kuwa jumla ya sh. milioni 463.59 zilitumwa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma na hazikuwa kwenye mpango wala bajeti ya Manispaa na hazijawahi kuombewa matumizi kama bajeti ya ziada,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live