Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumiaji mitandao ya kijamii watakiwa kuzingatia maadili

7cdd0ab0700545f495591ecaf79bbb43 Watumiaji mitandao ya kijamii watakiwa kuzingatia maadili

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni – Dar es Salaam, Sara Msafiri amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuzingatia maadili ya utoaji wa habari ili kuepuka kusababisha mtafaruku katika jamii kupitia mitandao yao hiyo.

Kauli hiyo ya Mkuu huyo wa Wilaya imekuja baada ya kutolewa kwa tafsiri tofauti kwenye mitandao ya kijamii inayokinzana na kile alichokimaanisha.

Taarifa hiyo inayopotosha inamnukuu akisema” Ni lazima umkatikie aliyekuletea hela, siyo kila mtu unamkatikia katikia tu, hamna kukatika katika hovyo, viuno vyenu viwekeni.”

Akizungumza na gazeti hili, Sara alibainisha kuwa hakuwa akimaanisha hivyo kama ilivyonukuliwa kwenye mitandao isipokuwa alimaanisha kuwa siyo kila muziki unaosikia unapaswa kuucheza kwa kuwa miziki mingine imelenga kuigawa jamii na kuongeza chuki.

Alisema kauli hiyo aliitoa kwenye hafla ya kuzungumzia maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano ambapo aliwaambia wananchi kuwa wacheze nyimbo zinazohusiana na maendeleo ya nchi na siyo zinazowagawa wananchi.

Alisema:”Hivyo niliwaambia wananchi kuwa wacheze kwa kuzikatikia viuno nyimbo zinazohusiana na maeendeleo kama vile zimeletwa barabara, maji na hospitali hapa lazima wananchi mkatike viuno kupongeza maana huyu anayeimbwa anakuletea maendeo naye ni Chama Cha Mapinduzi(CCM) ila siyo anayewagawa na kuwajengea chuki huyu unamkatikia nini.”

Sara alionesha kukerwa na watu wanaoishia kutumia mitandao ya kijamii kupotosha alichokimaanisha kwa kuwa siyo tu wamemkwaza yeye kama Mkuu wa Wilaya ila pia hawajawatendea haki wananchi kwa kuwapatia taarifa tofauti na kilichomaanishwa.

Alibainisha, katika sekta ya Habari na Mawasiliano kuna nguvu kubwa inayoweza kubadilisha maisha ya watu ambayo ni taarifa sahihi zinazoweza kuwahamasisha wananchi kuhusiana na nini wafanye kuchangia maendele na kama wakiendelea kuwepo wapotoshaji wa taarifa hizo maendeleo yanaweza kuchelewa.

Chanzo: habarileo.co.tz