Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumiaji maji Mufindi wapewa tahadhari

Maji Watumiaji maji Mufindi wapewa tahadhari

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau wa maji Wilaya ya mufindi mkoani Iringa wametakiwa kuchukua tahadhari ya utunzaji wa mazingira na kulinda vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na Mwananchi leo 13, 2023, Meneja wa Shirika la Water for Afrika, Nestory Sanga baada ya kumaliza wa kikao cha nusu mwaka cha vyombo vya watoa huruma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs) kilichoandaliwa na Ruwasa na kilichofanyika katika ukumbi wa Boma Wilayani hapa amesema changamoto kubwa sasa ni mabadiliko ya tabianchi.

“Changamoto kubwa kwa sasa hali ya mazingira kubadilika hatuwezi kujua miaka 10 paka 15 ijayo hali ya mazingira yatakuwa yameathirika kwa kiwango gani hivyo ni muhimu kuchukua hatua kutatua changamoto hii," amesema Sanga.

Aidha Sanga amesema maeneo mengi wamekuwa wakizalisha maji na kuwalipisha wateja wao huku wakiwa bado hawajatenga kiasi chochote kwa ajili ya kuendeleza vyanzo hivyo.

Amesema ni muhimu wadau na Serikali kuchukua sera hizo na kuzifanyia kwa ajili ya kuzibadirisha ili kusudi vyonzo hivyo viweze kuwa endelevu.

Pia, meneja huyo ameeleza shirika hilo limelenga kuwasaidia miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo kuanzia January mpaka Novemba jumla ya visima virefu 27 wamefanikiwa kuchimba wilayani hapa.

Mbali na hilo pia meneja huyo ameishukuru Mamlaka ya Usambazaji Maji Vijiji (Ruwasa) kwa namna ambavyo wameonyesha ushirikiano wao mara kwa mara kwa Shirika hilo katika utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.

Ofisa Uhamasishaji kutoka Taasisi ya Waandisi Tanzania (TAEEs), Sayuni Mbwiga amesema, utunzaji wa mazingira ni jambo la msingi hasa katika suala la maji kwa sababu usalama wa maji huanzia kwenye chanzo ili kuhakikisha vyanzo hivyo vinakuwa katika hali ya usafi.

"Ili kupata maji salama lazima kuzingatia suala la usafi wa mazingira kuanzia kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kuhakikisha vyanzo hivyo vinakuwa katika hali ya usafi," amesisitiza Mbwiga.

Mbwiga ametaja namna ambavyo wananchi wanaweza kutunza vyanzo hivyo visiweze kuchafuliwa ikiwemo kuacha kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na kulishia mifungo karibu na vyanzo hivyo ili waweza kutunza na kulinda vyanzo hivyo.

Meneja wa Ruwasa wilayani hapa, Mhandisi Happiness Mrisho amesema lengo la kikoa hicho ni kuwajengea uwezo Jumuiya za Watumia Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) ili waweze kupata uelewa zaidi ambayo utawasaidia katika miradi yao kuwa endelevu.

Mhandisi huyo amesema kuwa kwa sasa Wilaya hiyo inajumla ya Jumuiya za watumia maji 16 ambapo awali zilikuwa hazijawezeshwa vizuri hali ambayo ilipelekea zishindwe kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

"Kipindi cha nyuma jumaiya zetu zilikuwa zimetetereka katika utendaji kazi wake ilà kwa sasa tunashukuru hata makusanyo ya maduhuri ya maji yameongezeka kwa sababu wameweza kuajiri wasimamizi na wahasibu wa Jumuiya hizo," amesema Mhandisi Mrisho.

Hata hivyo, meneja huyo ameeleza mafanikio ambayo wameyapata katika miradi hiyo inatokana na usimamizi mzuri wa fedha ambavyo zinakusanywa kwa ajili ya kufanya ukarabati mbalimbali wa miradi ya maji pale inapohitajika kufanya ukarabati huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live