Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa warejesha nondo 100 zilizopotea hospitali Nachingwea

Vifaa Pc Data Watuhumiwa warejesha nondo 100 zilizopotea hospitali Nachingwea

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kufuatia ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa inayoanza leo katika Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, watuhumiwa waliosababisha upotevu wa nondo 135 za ujenzi ya wodi ya kisasa katika Hospitali ya Wilaya hiyo wameanza kurejesha nondo 100 kati 135.

Akizungumzia tukio la kurejesha vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Dk Charles Mtabho amesema watu wanaotuhumiwa kusababisha upotevu wa nondo 135 wameanza kurejesha ndono 100 baada ya uongozi wa wilaya kuwataka kufanya hivyo.

Mtabho akizumgumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ameema pamoja na upotevu huo kuripotiwa polisi lakini wao kama halmashauri wamewataka watuhumiwa kurejesha nondo hizo ili ujenzi uendelee.

" Nikweli Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi, lakini sisi kwa upande wetu tumewataka watuhumiwa ambao ni ofisa idara ya ujenzi, daktari wa Hospitali ya Wilaya na mlizi warejeshe mali zilizoibwa kwa njia ya utatanishi na uchunguzi ukikamilika kama ikibainika hawakuhusika tutawarejeshea mali hizi ila tunachotaka ujenzi uendele usisimame" alisema Dk Mtabho.

Amefafanua kuwa tukio la wizi na kupotea kwa vifaa hivyo lilibainika Agosti mwaka huu ambapo walibaini upotevu wa nondo 135 za ujenzi wa wodi hiyo ya kisasa unaotarajia kugharimu Sh183.89 milioni ambapo hadi sasa zimetumika Sh 61 zilitengwa na halmashauri kutokanana mapato yake ya ndani.

Dk Mtabho amesema kwamba kuna watumishi ambao sio waminifu kwani hawakutimiza wajibu wao vyema na kusabibisha shughuli za Serikali kukwama.

Ameongeza kuwa wanasubiri uchunguzi wa Jeshi la Polisi na watuhumiwa watakapo bainika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Akizumgumza kitendo hicho Aisha Salum mkazi wa Majengo wilaya Nachingwea amedai kuwaa suala la kurejesha vifaa hivyo kiini macho kwani wanamuogopa Waziri Mkuu kwa kuwa atakuwa na ziara wiki ijayo.

“Sisi tunajua kuwa bila kuja waziri mkuu nondo hizo tayari zilikuwa mali yao wasingeresha” amesema Aisha Saidi Makojogo amesema ubadhirifu wa mali ya umma unachangia wananchi kukosa imani na kusabibisha kuwa wagumu kuchangia miradi ya maendeleo.

"Tuna muomba waziri mkuu na viongozi wengine kuwawajibisha watendaji wasio kuwa wadilifu wanakatisha tamaa na moyo wa kuchangia miradi ya maendeleo wananchi na akifika angalie na miradi mbalimbali ikiwemo wodi ya mama na mtoto uliyofunguliwa na mwenge, amesema Saidi.

Chanzo: mwananchidigital