Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa wa kuuza dawa za kulevya watiwa mbaroni Arusha

Pingu?fit=800%2C445 Watuhumiwa wa kuuza dawa za kulevya watiwa mbaroni Arusha

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kukamata watuhumiwa 188 kwa makosa tofauti ikiwemo ya Wizi na usafirishaji wa Madawa za Kulevya.

Pia jeshi hilo limekamatwa na Bunda 542 za Mirungi zenye uzito wa kilo 298. Akitoa taarifa hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salvas Makweli leo amesema jeshi hilo lilifanya operesheni maalumu Oktoba 13, 2023 hadi Novemba 13, 2023 kwa lengo la kuwakamata watuhumiwa wanaojihusisha na matukio ya uhalifu na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

ACP Makweli amebainisha kuwa Novemba 12 katika maeneo ya Philips katika Halmashauri ya Jiji la Arusha walifanikiwa kumkamata Gilbert Joseph (33) mkazi wa Sinoni Jijini Arusha na Peter Waweru (33) mkazi wa nchi jirani wakiwa wanasafirisha Mirungi Bunda 542 zenye uzito wa kilogramu 298 kwa kutumia gari aina ya Isuzu (namba zimehifadhiwa).

Aidha amesema watuhumiwa wote wawili wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoani humo linawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Jeshi pia limewataka watu wanaojihusisha na uhalifu hususani madawa hayo ya kuacha biashara hiyo ambayo inaharibu vijana wengi kwani wataendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live