Watu wawili wameruhiwa vibaya na wengine zaidi ya 50 kunusurika kufa baada ya gari la abiria la kampuni ya Abood lenye namba za usajili za usajili T266 DDV waliokuwa wakisafiri kutoka Morogoro kuja Dar es Salaam kupinduka katika eneo la Ruvu wilayani Kibaha.
Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi ya leo wamesema gari lilipinduka baada ya dereva wa basi hilo kupita lori lililokuwa mbele yake bila tahadhari na kukutana na gari jingine na alipojaribu kulikwepa alishindwa kulithibiti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea ajali hiyo na idadi ya watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni wawili akiwemo dereva wa basi hilo na wengine waliokuwa katika basi hilo wamenusurika.
Amesema tayari amekiagiza kikosi cha usalama barabarani mkoani humo kuwatafuta madereva wa mabasi mawili mengine yaliyokuwa yanakimbizana na basi hilo jambo lililopelekea kutokea ajali hiyo.