WATU wawili wamekufa, huku wengine 28 wakinusurika baada ya kuvamia eneo la mgodi uliozuiliwa Kijiji cha Kanegere, wilayani Mbogwe mkoani Geita kufunikwa na kifusi.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo na kueleza ajali hiyo ilitokea Septemba 10, 2023.
Kamanda Jongo amewataja waliofariki ni mkazi wa mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, Justine Godwin (23) pamoja na mkazi wa wilayani Bariadi mkoani Shinyanga Wilson Masunga (23).
“Mgodi huu ulikuwa umefungwa na watu walikuwa wamezuiliwa kuingia kwenye mgodi huo. Hao watu ni maarufu kama manyani, walipita njia za panya na kuvamia ule mgodi kuanza kuchimba,” amesema Kamanda Jongo.