Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu watano wafa mdogini

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nyang'hwale. Wachimbaji wadogo watano wamepoteza maisha na wengine wanne wahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo wakati wakichimba dhahabu katika eneo la Mwasabuka wilayani Nyang'hwale mkoani Geita.

Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale, Hamimu Gwiyama amesema tukio hilo limetokea alfajiri juzi Alhamisi Novemba 29, 2018.

Amesema eneo hilo leseni yake inamilikiwa na mgodi wa Bulyanhulu na kwamba lilivamiwa na wachimbaji wadogo. 

Mkuu huyo wa wilaya amesema chanzo cha vifo hivyo ni maduara matano (mashimo) yaliyokuwa yanachimbwa kutitia na kuwafukia.

Amesema baada ya tukio hilo wachimbaji walifanya siri hadi leo Jumamosi Desemba 1, 2018 mchana diwani wa eneo hilo alipotoa taarifa kwa uongozi wa wilaya.

Amesema katika shughuli za uokoaji miili mitano imeopolewa na bado wachimbaji wengine wanne hawajapatikana.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa Gwiyama amesema uongozi wa wilaya umesimamisha shughuli za uchimbaji ili kuwatafuta ambao hawajapatikana lakini pia kuruhusu ukaguzi wa usalama ufanyike katika mashimo mengine yaliyopo kwenye eneo hilo.

Eneo la mgodi wa Mwasabuka lina watu zaidi ya 3,000 wanaojihusisha na uchimbaji mdogo.



Chanzo: mwananchi.co.tz