Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu saba wafariki ajalini Kilolo, wanne majeruhi

Tue, 23 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu saba wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Rav4 walilokuwa wakisafiria kugongana na bajaji katika Kijiji cha Ruaha Mbuyuni.

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah katika taarifa yake aliyoitoa amesema ajali hiyo imetoka jana jioni Ijumaa Aprili 20, mwaka huu.

 “Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari kushindwa kulimudu baada ya kuhama upande wake, mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Asia amesema katika ajali hiyo watu watano walifariki papo hapo na wawili ambao mmoja ni mjamzito walifariki baada ya kufikishwa katika kituo cha afya cha Mtanfika.

Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Sabaha Faraji (35) , Musa Ngwembele (58) miaka (58), Yohana Zemela (33), Kondo Chonongwa (20) na Tahea Kikunile (12) wote wakiwa wakazi wa kijiji cha Mtandika wilayani Kilolo.

Wengine ni Shangwe Kigula (18)mkazi wa Kijiji cha Nyazwa na Zena Kikunile (8) mkazi wa kijiji cha Mtandika.



Chanzo: mwananchi.co.tz