Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 9 waliozama kwenye boti Coco Beach wote wameokolewa

Legacy  2 25 Watu 9 waliozama kwenye boti Coco Beach wote wameokolewa

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Zimamoto Kinondoni, Dar es Salaam, Elisa Mugisha ametoa wito kwa wananchi kuwa wepesi kutoa Taarifa pale linapotokea tatizo au kuwepo na taarifa za matukio yanayohitaji uokoaji.

Amesema kwa mujibu wa taarifa walizopata ni boti hiyo ilizama majira ya mchana na taarifa zikawafikia baadaye sana.

Amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na vijana wa hapo Coco Beach maarufu kama Beach Boys wenye mafunzo maalumu ya uokoaji wamefanikiwa kuokoa watu wote waliokuwa katika boti hiyo.

Ameongeza kuwa boti hiyo iliyokuwa na watu Tisa wote wameokolewa na wapo salama.

"Ukiona tatizo lolote tupigie namba ya dharura 114 mara moja kwa simu yako hiyohiyo kwa maana watu walikuwepo wengi wanarekodi tukio (na simu zao) lakini taarifa kwetu zimechelewa kutufikia," Alisema Mugisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live