Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 9 wafa kwa kula nyama ya kasa Zanzibar

Kasa 1 Watu 9 wafa kwa kula nyama ya kasa Zanzibar

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto 8 na mwanamke mmoja wamefariki dunia baada ya kula nyama ya Kasa Visiwani Zanzibar.

Mamlaka visiwani humo zimeripoti kuwa watu 78 wamelazwa hosptali baada ya kula nyama hiyo ambayo hupendwa sana Zanzibar.

Ulaji wa nyama hiyo ikiwa si salama husababisha sumu inayoweza kuua. Hali hiyo haina dawa bali yapo matibabu ya kuweza kusaidia tu hali za waathirika.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Haji Bakari amesema kuwa vipimo vya maabara vimeonyesha kuwa wote walioathirika walikula nyama ya Kasa siku ya Jumanne.

Dkt. Bakari aliongeza kuwa Mwanamke aliyefariki siku ya Ijumaa ni Mama wa mmoja wa watoto waliofariki mwanzoni mwa wiki.

Mamlaka zimepeleka timu ya usimamizi wa maafa inayoongozwa na Hamza Hassan Juma Kisiwani Zanzibar. Vilevile watu wameonywa kutokula nyama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live