Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 700 waondolewa hifadhini Singida

Pori Chaka TFS Singida

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu zaidi ya 700 waliovamia Msitu wa Hifadhi ya Mgodi uliopo wilayani Singida wameondolewa huku silaha mbalimbali zikikamatwa na miongoni mwao wamefunguliwa mashtaka.

Kamanda wa kikosi kasi kilichoundwa kuwaondoa wavamizi hao, Tumaini Membi alisema shughuli ya kuwaondoa wavamizi hao ilifuata utaratibu maalumu ikiwamo kuwasomea dodoso linalowataka kuondoka Hifadhi kwa kuishi na kufanya shughuli za kiuchumi kinyume cha sheria.

Katika maelezo aliyoyatoa mbele ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Profesa Dos Santos Silayo aliyeambatana na Kamanda wa Kanda ya Kati wa TFS, Mathew Kiondo mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema wamekumbana na changamoto mbalimbali katika kazi hiyo iliyoanza Desemba 3, mwaka jana ikiwemo kurushiwa mishale mara mbili na wavamizi hao.

Hata hivyo, Tumaini alisema kikosi chao kinachojumuisha polisi, askari wa Suma JKT na TFS kilisimama imara kuhakikisha kuwa kinawaondoa watu hao sambamba na mifugo na mali zao.

"Lakini katika operesheni hii tulikamata silaha mbalimbali kama mishale 75, pinde 12, mikuki 22, mapanga 33, fimbo 150 na visu vitano," alisema.

Mbali na silaha, kiongozi huyo wa kikosi kazi alivitaja vitu vingine walivyokamata kuwa ni majembe ya mkono 10, majembe ya kukokota na ng'ombe manane, mbegu za mahindi kilo 21 na misumeno 10 ikiwemo ya kuchania mbao.

"Watuhumiwa watatu tuliwakamata baada ya kurejea hifadhini kuendelea na shughuli zao ikiwamo kujiandaa kwa ajili ya shughuli za kilimo," alisema Tumaini na kwamba wamefunguliwa mashtaka tofauti polisi mjini Singida.

Hata hivyo alisema wavamizi wengi walioondolewa wameweka makazi katika vijiji jirani na msitu ambapo wamekuwa wakiingiza mifugo yao hifadhini jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu kiongozi huyo, kaya 411 zenye watu zaidi ya 700 zilikuwa zikiishi hifadhini na kuendesha shughuli za kilimo, ufugaji na ukataji miti kwa ajili ya mkaa, ambapo wamefanikiwa kuharibu makazi 381 ya watu hao huku kazi ya kuharibu yaliyobaki ikiendelea umaini alipendeleza doria za mara kwa mara ziendelee kufanyika hifadhini ili wavamizi wasirejee upya na pia kudhibiti mifugo isiingie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live