Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 7 washambuliwa na Fisi Tarime

Fisi Kiganja Watu 7 washambuliwa na Fisi Tarime

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu saba wakazi wa Mtaa wa Bugosi, katika Halmashauri ya Mji wa Tarime wakiwamo watano wa familia mbili tofauti, wamelazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa na fisi.

Watu hao Francis Siongo, Joseph Siongo, Seta Saro, Anna Saro, Slia Saro na Mang'enyi Chacha, walikutwa na mkasa huo wakiwa njiani kwenda shambani kulima.

Wakisimulia tukio hilo wakiwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime juzi, baadhi ya majeruhi hao walioweza kuzungumza walisema fisi huyo aliwavamia alfajiri wakiwa njiani.

Francis Siongo na Seta Ngoncho walisema kwa nyakati tofauti kuwa mkasa huo uliwakuta saa 11:00 jana wakienda kwenye mashamba yao yaliyoko Nyandoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live