Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 7 wafariki dunia kwa kupigwa na radi

Radu 14 Wwsjeruhiwa na radi hiyo

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu saba wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi katika maeneo tofauti katika Wilaya za Nkasi na Sumbawanga mkoani Rukwa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nkandasi, Given Kisantola amesema tukio la kwanza lilitokea Februari 26 saa 9 alasiri Kijiji cha Nkandasi wilayani Nkasi.

Watano waliokuwa wakifanya kibarua cha kupanda maharage shambani walikufa papo hapo huku 14 kati yao walijeruhiwa baada ya kupigwa radi wakiwa wamejikinga kwenye nyumba kidogo iliyopo shambani humo.

Amesema kuwa watu hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao, baada ya kuona mvua imeanza kunyesha waliacha kupanda maharage na kuamua kukimbilia kwenye nyumba hiyo ili kujikinga na mvua.

Amesema, wakati watu hao wakiwa wamekaa ndani ya nyumba hiyo, ghafla radi ilipiga na kusababisha vifo hivyo na kujeruhi wengine waliokuwa wamejikinga mvua katika nyumba hiyo.

Mtendaji huyo amesema kuwa waliofariki ni wanaume watatu na wanawake wawili ambapo majeruhi walikimbizwa katika Zahanati ya jeshi Milundikwa kwa ajili ya matibabu na wengi wao wanaendelea vizuri huku wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Ambao ni yusuph mbalamwezi (24), Leonard Wayomba (21) Flansisco Kangama, Fazil wayomba (24) Shukuru Mutayagwa (28) na mtoto Abinet Kazumba (8).

Amewataja pia majeruhi kuwa ni pamoja na Veronica Saanane(27), Fobi Mbonile(28) Solostina Sokoni (39), Edina Noel (39) Getruda Mwananjela (34) mtoto Tatu Miyula (10) Teddy Wazamani (37), Mary Kauzeni (18)Daniel Kamilembe (19) Lenatha Chakula (51) Magreth Savery (40),Retisiya Fataki (38) na Veronica Swaila (27).

Aidha, katika tukio jingine tukio jingine lililotokea siku hiyo hiyo mwanaume mmoja ambaye jina lake halijajulikana mkazi wa kijiji cha Luwa Manispaa ya Sumbawanga, amekufa papo hapo yeye na mtoto wake baada ya kupigwa radi wakiwa shambani wanalima.

Kamanda Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live