Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 57 washikiliwa tuhuma za mauaji ya watoto Simiyu

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lamadi. Watu 57 wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi kuhusiana na matukio ya mauaji ya watoto wa kike yanayohusishwa na imani za kishirikina katika eneo la Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Kukamatwa kwa watu hao ni matokeo ya kura za maoni na ziara ya hivi mkoani Simiyu ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro aliyetangaza oparesheni siku 10 ya kuwanasa watuhumiwa wa mauaji hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la Lamadi juzi, Kiongozi wa Oparesheni hiyo ya polisi, Salum Amdun alisema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya operesheni ya siku tatu.

“Miongoni mwa wanaoshikiliwa wamo waganga wa kienyeji na wapiga ramli chonganishi,” alisema Hamdun

Februari 14, 2019, wakazi wa Lamadi walipiga kura za siri zilizosimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Busega, Tano Mwena kuwabaini wanaohisiwa kuhusika na matukio ya mauaji ya watoto wa kike yanayotikisa eneo hilo tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Kabla ya tukio la kupiga kura, Februari 11, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alikubali ombi la wakazi wa eneo hilo la kupiga kura za siri kuwataja watuhumiwa.

Baada ya kura hizo, Mtaka aliahidi kuwa zitahesabiwa na kuchambuliwa na askari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Magereza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Uhamiaji na Polisi ambayo hata hivyo baadhi yao walinyooshewa vidole na wananchi kuwa wanahusika kwa kuwaachia watuhumiwa wanaokamatwa bila kuwafikisha mahakamani.



Chanzo: mwananchi.co.tz