Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Flight Link 5H Flight Link 5H – FLI.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea leo Jumatano katika Hifafhi ya Taifa ya Serengeti.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Uhifadhi Mkuu Kitengo cha Mawasiliano, Catherine Mbena imesema ajali hiyo imetokea jana Februari 28, 2024 majira ya saa 6:52 mchana kwa kuhusisha ndege ya kampuni ya Flight Link 5H – FLI.

Amesema ajali hiyo imetokea wakati ndege hiyo ikitua katika kiwanja cha ndege cha Kogatende kilichopo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

“Chanzo cha ajali ya ndege hiyo bado hakijajulikana. Abira wote watatu na rubani mmoja wako salama. TANAPA, itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu ajali hii,” amesema Mbena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live