Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 2,815 wanaopisha mradi wa umeme Arusha-Manyara wamelipwa

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Watu 2,815 wanaopitiwa na mradi wa usafirishaji umeme wa msongo wa KV 400 kutoka Namanga kupitia Arusha katika wilaya za Arusha, Monduli, Babati na Hanang’ wamelipwa hadi Machi mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatatu, Aprili 8, 2019 na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Babati Mjini (CCM) Pauline Gekul.

Gekul alitaka kufahamu ni wananchi wangapi wanaodai fidia ya maeneo yao yaliyopitiwa na mradi wa umeme wa KV 400 katika jimbo la Babati Mjini watalipwa.

Akijibu swali hilo, Mgalu amesema ulipaji fidia ulianza Agosti mwaka jana baada ya kukamilika kwa zoezi la uthamini na uhakiki wa mali na mazao yatakayoathirika na utekelezaji wa mradi.

Amesema hadi Machi mwaka huu, zaidi ya Sh31.87bilioni zimeshalipwa kwa watu 2,815 kutoka wilaya za Arusha, Monduli, Babati na Hanang.

“Kwa upande wa Wilaya ya Babati fedha zaidi ya Sh6.28bilioni zimeshalipwa kwa wananchi 995 hadi kufikia mwishoni mwa Machi 2019,” amesema.

Amesema wananchi 86 waliobaki wakati wowote watalipwa fedha zao Sh638 milioni baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki unaoendelea.



Chanzo: mwananchi.co.tz