Wananchi 12,158 wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, wanaishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) huku nusu yao wakiwa ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24.
Mratibu wa UKIMWI wa Halmasahauri ya Rungwe, George Mashimba amesema kati ya idadi hiyo ya wanaoishi na maambukizi, vijana ni 659 sawa na asilimia 5.4 huku vijana wa kike wakiwa wengi zaidi.
Amesema wasichana ni 467 huku wa kiume wakiwa 192 pekee jambo ambalo linahitaji nguvu zaidi ya kukabiliana na ongezeko la maambukizi kwa vijana.
Amesema hali ya maambukizi ya VVU katika wilaya hiyo ni mbaya na hivyo akawataka wadau mbalimbali kuungana na Serikali katika kukabiliana na tatizo hilo.