Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 1,404 waathiriwa na mafuriko Morogoro

Shaka Kilosa Mafuriko (600 X 278) Watu 1,404 waathiriwa na mafuriko Morogoro

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya watu 1,404 wameathirika na mafuriko katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro huku nyumba 351 ziingia maji na vyoo 368 kubomoka. Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amesema hayo jana Jumatano Machi 20, 2024 na kuongeza kuwa nyumba 17 zimebomoka.

Shaka amesema nyumba zilizobomoko tano zinatoka Kitongoji cha Kampala, nyumba nane Kitongoji cha Estate na nyumba nne Kitongoji cha Madizini. Amesema jumla ya vyoo 368 vimeathirika kutokana na mafuriko, hivyo kufanya maji kuwa machafu baada ya vyoo hivyo kubomoka.

Shaka amesema jumla ya visima 30 vya maji vinavyotumika vimeathirika na mafuriko hayo kwa kuingiliwa na maji machafu.

Kuhusu hali ya miundombinu ya barabara, Shaka amesema maji yameharibu zaidi ya kilometa 170 za barabara na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Kilosa na Mikumi.

Amesema Machi 17 mwaka huu maji mengi yalijaa katika Mto Miyombo unaopita vijiji vya Ulaya, Zombo na Changarawe baada ya mvua kubwa kunyesha katika vijiji vya Kisanga, Madizini na Kitunduweta.

Amesema mvua hiyo ilisababisha athari katika makazi, mashamba, miundombinu ya maji na barabara katika maeneo hayo.

Shaka amefafanua kuwa Kijiji cha Changarawe kimekuwa na matukio ya kupatwa na mafuriko tangu mwaka 2016 na msimu huu wa mvua kuanzia Desemba mwaka jana.

“Mafuriko haya yamesababishwa na maji kujaa katika Mto Miyombo nje ya kingo za mto baada ya ongezeko la kujaa mchanga katika mabwawa ya Nara na Kipera yaliyochimbwa kwa ajili ya kupunguza kasi ya maji kipindi cha mvua kubwa na kuruhusu maji machache kuingia katika mto huo,” amesema Shaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live