Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto yatima ni jukumu la kila mmoja

55668 Pic+yatima

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Pamoja na jamii kuwapelekea misaada mbalimbali watoto yatima, mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na utoaji wa elimu ya kisukari ya Dicoco,  Lucy Johnbosco amesema watoto hao wanahitaji elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza.

Akizungumza leo Mei 4  baada ya kukabidhi misaada mbalimbali kwenye kituo cha watoto yatima cha Hisani kilichopo Mbagala, Dar es Salaam,  Lucy amesema kisukari ni ugonjwa unaoweza kuwapata watoto pia.

Katika hafla hiyo, mfanyakazi wa Mwananchi Communications Ltd, Lilian Masanche pia alikabidhi zawadi mbalimbali kwenye kituo hicho wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Lucy amesema jamii inao wajibu kuhakikisha usalama wa watoto hao ili wafikie ndoto zao kimaisha.

"Taasisi yangu imeleta vitabu kuhusu namna ya kujilinda na magonjwa yasiyo kuambukizwa, mara nyingi tunapokuja kuwaona hawa watoto huwa tunasahau afya zao na hili ni jukumu la kila mmoja," amesema.

Kwa uapnde wake, Lilian amesema siku yake ya kuzaliwa imekuwa na maana zaidi baada ya kuwatembelea na kuwaona  yatima.

"Siku nyingine zote nilikuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa kukata na kula keki lakini leo nafutahi kuwa na watoto ambao wanahitaji malezi na upendo wetu," amesema.

Naye Ofisa Masoko wa Kiwanda cha Dawa cha Keko, alisema watoto yatima wanahitaji huduma bora za afya kama walivyo watoto wengine ili ukuaji wao usiwe na matatizo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Hisani cha Mbagala, Hidaya Mtalemwa amesema watoto yatima70 walio kwenye kituo hicho wanahitaji misaada mbalimbali hasa chakula na mavazi.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz