Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili walioteketea kwa moto wazikwa

Aboud Msgz Watoto wawili walioteketea kwa moto wazikwa

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameongoza mamia ya wananchi wa Kata ya Lukobe kwenye mazishi ya watoto wawili wafamilia moja waliopoteza maisha baada ya moto kuteketeza nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa Mei 4, 2024.

Watoto hao wakiume ni Brown George Banzi mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi Msamvu A na Bright George Banzi mwenye umri wa miaka minne na mwanafunzi wa shule ya awali

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kibao cha Shule Tushikamane, Kata ya Lukobe, Omary Hassan amesema kuwa wakati nyumba hiyo inaungua moto wazazi wote wawili hawakuwapo nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live