Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wafariki ndani ya dimbwi la maji

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Watoto wawili wamefariki dunia kwenye dimbwi lililochimbwa kwa ajili ya  udongo wa kujengea barabara.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Kigwa B wilayani Uyui, mkoa wa Tabora.

Diwani wa Kigwa, Wiston Msemo amesema walipata taarifa ya kupotea kwa watoto hao wawili usiku na kuanza kuwatafuta pasipo mafanikio.

Alisema baada ya jitihada kubwa za kuwatafuta, miili ya watoto hao, Salima Omar (9) na Hadija Ramadhani (5) imekutwa kwenye dimbwi la maji  lililotokana na kuchimbwa  udongo wa ujenzi wa barabara ya Tabora hadi Nyahua kwa kiwango cha lami.

Baba mzazi wa Salima, Omar Hamis amesema mtoto wake alienda kucheza na wenzake na baadaye kutoonekana na mwenzake aliyefariki naye na kuanza kuwatafuta hadi saa 7:00 usiku bila mafanikio.

"Tulipata taarifa kuwa mmoja ameonekana akielea kwenye dimbwi la maji tulipoenda tukakuta amefariki na mwenzake alikuwa amekufa chini ya dimbwi," alisema.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema kipindi hiki cha masika wazazi na walezi wanapaswa kuwa macho na watoto wao na kutoacha nyumba zao pasipo ulinzi ili kunusuru watoto na mali zao.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz