Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wafariki kwa kukosa hewa ndani ya gari

Watoto Wawili Wafariki Kwa Kukosa Hewa Ndani Ya Gari Watoto wawili wafariki kwa kukosa hewa ndani ya gari

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: Malunde

Watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 6 na 7 wamefariki dunia kwa kukosa hewa wakichezea gari katika Kitongoji Ng’ung’ula Kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Jomu, Juma Warioba na Diwani wa kata ya Tinde, Japhar Kanolo wamesema tukio hilo limetokea Jumanne Agosti 22,2023 majira ya saa 12 jioni wakati watoto wakicheza ndani ya gari likajifunga na wazazi wao hawakujua kilichokuwa kinaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo.

“Jeshi la polisi tumepokea taarifa hizi. Wazazi walitoka Mwanza wakiwa na gari lao kwenda kusalimia nyumbani kwao Tinde, walipofika pale hawafunga milango ya ile gari, na vioo vilikuwa vimefungwa”,amesema Kamanda Magomi.

“Kilichotokea ni watoto walienda kucheza kwenye lile gari, wakalikorofisha likawa likajifunga. Kwa mujibu wa Daktari watoto wale walifariki kwa kukosa hewa”,ameeleza Kamanda Magomi.

Chanzo: Malunde