Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wafa maji Mkuranga

Watu Saba Wahofiwa Kufariki Baada Ya Kuvuka Mto Uliofurika Kenya Watoto wawili wafa maji Mkuranga

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wawili wamefariki dunia baada ya kuzama katika Maji wakiwa na wazazi wao maeneo ya Churwi karibu na Mto Mzinga Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani baada ya kuzama darajani.

Watoto hao mmoja mwenye mwaka mmoja na miezi mitatu na mwingine mwenye miaka minne wamefariki wakitokea upande mmoja wa daraja wakirudi nyumbani kwao.

Baada ya tukio hilo Mbunge wa Jimbo la Mkuranga na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega aliambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo Khadija Nasir walifika eneo hilo kutoa pole.

Viongozi hao walitoa pole kwa wafiwa pamoja na kuongeza nguvu ya kuendelea na jitihada za utafutaji wa mtoto wa miaka minne ambaye mpaka sasa hajapatikana.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Francisca Chunji ameeleza jitihada bado zinaendelea za kutafuta mtoto wa miaka minne ambapo mpaka sasa hajapatikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live