Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wa familia moja wateketea kwa moto Moshi

Moto Ghnn Watoto wawili wa familia moja wateketea kwa moto Moshi

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wawili ambao ni wa kike na kiume, wenye umri wa miaka miwili na nusu na mwingine miaka miwili na miezi minne katika Kijiji cha Shinga, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wameteketea kwa moto baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuungua.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Februari 28, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea leo watoto hao wakiwa wamelala wakati baba yao alipoenda dukani kununua sigara.

"Baba wa hawa watoto aliondoka muda mfupi kwenda kununua sigara dukani wakati anarudi akakutana na moshi mkubwa ukitoka ndani ya nyumba hiyo, ambapo watoto wote wawili walioteketea kwa moto," amesema Kamanda Maigwa.

Aidha, Kamanda Maigwa amesema chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live